UJUE UISLAAMU HALISI
Assalaam
Alaykum,baada ya kuyajua hayo tuliyoyajua kuhusiana na NINI UISLAAM NA
NANI NI MUISLAAM,NA NANI SI MUISLAAM.Leo tuendelee na kipengele kingine
cha maana ya neno DINI.UISLAAM huliangalia neno Dini kwa maana
iliyotofauti na waichukuliayo Wasiokuwa Waislaam!Wasiokuwa Waislaam
hulichukulia neno Dini kwa maana ya Imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi
Mungu.Kwa mfano katika Katika Kamusi ya Kiingereza ya A.S Horbi with A.B
Lowide,A.C Gimson,Oxford Advanced Leaner's Dictionary of current
English,Oxford University Press,Nairobi(1962) Ukurasa wa 713,neno
Religion(Dini) limefasiriwa hivi "Beliefin the existence of Supernatural
ruling power,the Creator and Controller of the universe,Who has given
to Man a Spiritual nature which continues to exist after the death of
the body"
Tafsiri yake ni kuwa "Dini ni Imani ya kuwepo Mungu
Muumba,aliye Muweza na Mwenye Nguvu juu ya kila kitu.Mmiliki wa
Ulimwengu ambaye amempa Binaadamu Roho ambayo huendelea kuishi baada ya
kifo cha mwili"
Aidha katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu neno Dini
limetafsiriwa kama ifuatavyo "Imani inayohusiana na Mambo ya kiroho
baina ya Binaadamu na Mwenyezi Mungu,au njia ya kuhusiana na Mwenyezi
Mungu".Kwa tafsiri hizi Makafiri wao hudai kuwa hawana Dini kwa kuwa
hawana Imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.
Lenin mmoja wa wasomi
wa Kikafiri anasema "Every body must be absolutely free to profess any
Religion he pleases or no Religion whatever,i.e to be a Atheist which
every socialist is as a rule...." Tafsiri yake ni kuwa "Kila Mtu hana
budi kuwa huru kabisa kufuata Dini yoyote anayoitaka au asiwe na Dini
kabisa,yaani awe Kafiri,jambo ambalo inambidi kila mjamaa awe hivyo...."
Neno Dini katika Lugha ya Kiarabu hufasiriwa kama Mila,Utamaduni,Desturi,Njia,Utratibu
au Mfumo fulani.Katika Uislaam Neno Dini maana yake ni "Utaratibu au
Mfumo wa Maisha ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu au Kiumbe".Kwa maana hiyo
hakuna Mtu asiyekuwa na Dini kwani ni lazima Mtu awe amefuata utaratibu
fulani ambao aidha amejipangia mwenyewe au amepangiwa!
Na kwa
mtazamo wa Uislaam Dini(Mifumo ya Maisha) ipo mingi tu,ndio maana Mtume
aliambiwa aseme kuwaambia Makafiri kuwa "NYINYI MNA DINI YENU,NA MIMI
NINA DINI YANGU"(Sura ya 106 Aya ya 6).Kwa maana nyingine Mtume alikuwa
akiwaambia kuwa "NYINYI MNA MFUMO WENU WA MAISHA,NA MIMI NINA MFUMO
WANGU WA MAISHA"Tofauti ni kuwa Mfumo aliokuwa akiufuata Mtume umetungwa
na Mwenyezi Mungu mwenyewe na Mfumo waliokuwa wakiufuata Makafiri
walijitungia wenyewe!
"INNAD DIINA INDALLAAHIL ISLAAM..."Mwenyezi
Mungu ananadi kupitia kinywa cha Mtume(s.a.w),yenye Tafsiri kwamba
"HAKIKA DINI INAYOKUBALIKA MBELE YA MWENYEZI MUNGU NI UISLAAM"(Sura ya 3
Aya ya 19).Ukiyakunjua zaidi maneno hayo kwa maana ya neno Uislaam na
neno Dini tulizokwishaziona ni kuwa "HAKIKA MFUMO WA MAISHA UNAOKUBALIKA
MBELE YA MWENYEZI MUNGU NI WAKUTII NA KUNYENYEKEA AMRI,SHERIA NA HUKUMU
ZA MWENYEZI MUNGU"
Na kwa kumalizia somo letu kwa Siku ya
leo,namalizia kwamba "NA ANAYETAFUTA DINI ISIYOKUWA YA
UISLAAM,HAITOKUBALIWA KWAKE.NAYE AKHERA ATAKUWA NI MIONGONI MWA WENYE
HASARA"(Sura ya 3 Aya ya 85).Nayo tukiikunjua inakuwa "NA ANAYETAFUTA
MFUMO WA MAISHA USIOKUWA WA KUTII NA KUNYENYEKEA AMRI,SHERIA NA HUKUMU
ZA MWENYEZI MUNGU,HAUTOKUBALIWA KWAKE.NAYE AKHERA ATAKUWA NI MIONGONI
MWA WENYE HASARA"
Shime ndugu zangu tuishi katika Utaratibu na Mfumo aliouridhia Allah!
"SOMO LITAENDELEA INSHAALLAH......."
No comments:
Post a Comment