Assalaam
Alaykum, Kumbukeni kuwa
huu ni Uwanja mpana unaruhusiwa kutoa maoni yako kwa namna
ulivyojaaliwa ili mradi usimtukane Mtu wala kumdhalilisha!Ndugu zangu
tutumie Akili na Fikra zetu,laa sivyo tutaenda kuhukumiwa kwa hilo!ALLAH
anasema "NA KWA HAKIKA TUTAWAINGIZA JAHANNAM WENGI KATIKA MAJINI NA
WATU.WANA MIOYO LAKINI HAWAFAHAMII KWAYO,NA WANA MACHO LAKINI HAWAONI
KWAYO,NA WANA MASIKIO
LAKINI HAWASIKII KWAYO.HAO NI KAMA WANYAMA BALI WAO WAMEPOTEA ZAIDI.HAO NDIO WALIOGHAFILIKA"(Sura ya 7 Aya ya 179).
Akasema tena kuwa "HIKI (QUR'AN) NI KITABU TULICHOKITEREMSHA KWAKO ILI
ZIZINGATIWE AYA ZAKE NA ILI WAKUMBUKE WENYE AKILI"(Sura ya 38 Aya ya
29).Na namalizia kwa kauli yake kuwa "......NA(MWENYEZI MUNGU) HUJAALIA
UCHAFU KWA WALE WASIOTUMIA AKILI"(Sura ya 10 Aya ya 100).Aya zote hizo
zinaonesha umuhimu wa utumiaji wa Akili na Fikra zetu katika kuyaendea
mambo ya msingi,kwani ndicho kitu kinachomtofautisha Mwanaadamu na
Wanyama wengine!Haiwezekani wakati wa Usiku Mtu akwambie kuwa huu ni
Mchana nawe ukubaliane nae pasi na kufikiri!
Lakini vilevile,nilitoa
Dondoo za udadisi ambazo zingemsaidia Mchangiaji katika kutoa maoni
yake!Kwamba ikiwa Muongozo umekemea vikali juu ya Madhehebu(Makundi) na
kuiorodhesha kuwa ni Ukafiri na Ushirikina,na ikiwa Mtume(s.a.w)
hakuacha hali ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam!Je nini
kilichosababisha hali hii ya umakundi ndani ya Uislaam?
Dodoso
lingine likasema,Je hali hii ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam
inaweza kuondoka na Dini kurudi kama wakati wa Enzi za Mtume(s.a.w)?
Somo litaendelea inshaallah....!
Akasema tena kuwa "HIKI (QUR'AN) NI KITABU TULICHOKITEREMSHA KWAKO ILI ZIZINGATIWE AYA ZAKE NA ILI WAKUMBUKE WENYE AKILI"(Sura ya 38 Aya ya 29).Na namalizia kwa kauli yake kuwa "......NA(MWENYEZI MUNGU) HUJAALIA UCHAFU KWA WALE WASIOTUMIA AKILI"(Sura ya 10 Aya ya 100).Aya zote hizo zinaonesha umuhimu wa utumiaji wa Akili na Fikra zetu katika kuyaendea mambo ya msingi,kwani ndicho kitu kinachomtofautisha Mwanaadamu na Wanyama wengine!Haiwezekani wakati wa Usiku Mtu akwambie kuwa huu ni Mchana nawe ukubaliane nae pasi na kufikiri!
Lakini vilevile,nilitoa Dondoo za udadisi ambazo zingemsaidia Mchangiaji katika kutoa maoni yake!Kwamba ikiwa Muongozo umekemea vikali juu ya Madhehebu(Makundi) na kuiorodhesha kuwa ni Ukafiri na Ushirikina,na ikiwa Mtume(s.a.w) hakuacha hali ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam!Je nini kilichosababisha hali hii ya umakundi ndani ya Uislaam?
Dodoso lingine likasema,Je hali hii ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam inaweza kuondoka na Dini kurudi kama wakati wa Enzi za Mtume(s.a.w)?
Somo litaendelea inshaallah....!
No comments:
Post a Comment