MUENDELEZO WA SOMO LA MADHEHEBU
Assalaam
Alaykum!Naam tuendelee na
kufahamishana mawili matatu kuhusiana Uislaam!Baada ya kuona makemeo ya Allah juu
ya kuigawanya Dini na kuwa Makundi Makundi(Madhehebu) kwa kutuonesha
kuwa kufanya hivyo ni Ukafiri na ni Ushirikina!Tuone basi ni kipi hicho
CHANZO CHA MADHEHEBU KATIKA UISLAAM!Jambo ambalo ndio Mada ya Siku yetu
ya leo!
Ndugu zangu,Njama za kuugawa Uislaam hazikuanza jana wala
juzi,bali tangia Enzi za Bwana Mtume Muhammad(s.a.w).Jambo hilo la
kuigawa Dini lilikuwa likifanyika kila mara anapoletwa Nabii/Mtume wa
Mwenyezi Mungu kwa lengo la wale wenye kutawala waendelee kuwatawala
Watu ambao wakishaujua Ukweli kuhusiana na Maisha yao kwa ujumla
hawatokuwa na njia nyingine ya kuwatawala.
Jambo hilo ililazimu wale
wanaotaka kuendelea kutawala,wapambane na Manabii wa Mwenyezi Mungu kwa
kuiviza na kuifahamisha vingine ile Haki iliyokwisha kuja kwa lengo lao
hilo.Sitaki tuzame sana huko lisije Somo letu likawa refu sana hata
Msomaji akashindwa kuzingatia!Turudi sasa katika kuangalia hizo njama
zilizokuwa zikifanyika wakati wa Uhai wa Mtume(s.a.w) ili kuwagawa Watu!
Kitu cha Mwanzo walichofanya ni kuwaelekeza Watu na kuwapa mafunzo
kinyume cha yale aliyokuwa akifundisha yeye Mtume,na hayo yalifanywa na
wale Wanafiki waliokuwa wakijifanya kuwa ni Wanafunzi watiifu wa Mtume
hali ya kuwa ni waongo!Hayo Mtume hakuwa akiyajua mpaka alipozinduliwa
na Mwenyezi Mungu mwenyewe! "NA WANASEMA TUMETII,NA WANAPOTOKA KWAKO
KUNDI MOJA MIONGONI MWAO HUPANGA NJAMA USIKU KINYUME CHA YALE
UNAYOYASEMA..." (Sura ya 4 Aya ya 81).
Hawa walikuwa pamoja na
Mtume!Wanasikiliza Aya za Mwenyezi Mungu mbele ya Mtume(s.a.w) mwenyewe
kisha kumbe wanakuwa hawajaridhika na yale waliyofundishwa na Mtume,na
kuamua kukaa vikao vya mapinduzi usiku kupindua yale alowafundisha
Mtume!
Wafanya mapinduzi wa kabla ya Mtume walikuwa wakiyaingilia
moja kwa moja yale Mafundisho ya Kitabu husika na kuyachakachua!ndivyo
ilivyofanywa Taurati,Zaburi na Injili!lakini wafanya mapinduzi hawa wa
zama za Mtume Muhammad(s.a.w) walikumbana na mkwamo,pale walipokumbana
na Ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba "HAKIKA SISI NDIO TULIOUTEREMSHA
UKUMBUSHO(QUR'AN) NA HAKIKA SISI NDIO TUTAKAOULINDA"(Sura ya 15 Aya ya
9)
Kwahiyo zoezi la kutia mafundisho yao ndani ya Kitabu cha
Mwenyezi Mungu ili wapate kuwagawa Watu na kuendelea
kuwatawala,likagonga mwamba!hata hivyo hawakukata tamaa,wakaona ni bora
wamvae Mtume mwenyewe "NA WANAPOSOMEWA AYA ZETU ZILIZO WAZIWAZI,WALE
WASIOTARAJI KUKUTANA NASI HUSEMA:LETE QUR'AN ISIYOKUWA HII AU
IBADILISHE!SEMA:HAINIFALII MIMI KUIBADILISHA KWA ITAKAVYO NAFSI
YANGU.MIMI SIFUATI ILA NINAYOFUNULIWA. HAKIKA MIMI NAOGOPA IKIWA
NITAMUASI MOLA WANGU,ADHABU ILIYO KUU"(Sura ya 10 Aya ya 15).
kwa
hiyo Jaribio lingine likakwama!Ndio ikawabidi sasa waingie kazini
wenyewe kila Mtume anapofundisha hivi wao hutunga mengine ili
kuwadanganya Watu na kuwatoa kwenye mstari ili waendeleze mambo yao
waliyokuwa nayo kabla ya Mtume Muhammad kupewa Utume!Mwenyezi Mungu
anatupa habari kwamba hali hiyo ya kumbadilishia maneno illikuwa
ikimhuzunisha sana Mtume,hali iliyomlazimu Mwenyezi Mungu amtulize Mtume
wake kwa kumwambia "EWE MTUME!WASIKUHUZUNISHE WALE WAFANYAO HARAKA
KUKUFURU,MIONGONI MWA WANAOSEMA KWA VINYWA VYAO:TUMEAMINI NA HALI NYOYO
ZAO HAZIJAAMINI,NA MIONGONI MWA MAYAHUDI,WANAOKUSIKILIZA ILI WAKASEME
UWONGO,WANAOKUSIKILIZA KWA AJILI YA WATU WENGINE
WASIOKUFIKIA.HUBADILISHA MANENO KUTOKA MAUDHUI YAKE..."(Sura ya 5 Aya ya
41)
Hiyo ndio kazi waliokuwa wakiifanya baadhi ya Wanafiki miongoni
mwa Maswahaba wa Mtume wakishirikiana na Mayahudi,kutunga Maneno
tofauti na alivyofundisha Mtume mwenyewe kama alivyoteremshiwa na Mola
wake!Je Maswahaba hawa wazusi tutawajuaje hali ya kuwa Mtume Mwenyewe
hakuwa akiwajua!"NA KATIKA MABEDUI WALIO PEMBEZONI MWENU KUNA
WANAAFIKI,NA KATIKA WENYEJI WA MADINA PIA KUNA WALIOBOBEA KATIKA
UNAAFIKI,WEWE HUWAJUI.SISI TUNAWAJUA.TUTAWAADHIBU MARA MBILI KISHA
WATARUDISHWA KATIKA ADHABU KUBWA"(Sura ya 9 Aya ya 101).
Alaa kumbe
miongoni mwa Maswahaba wa Mtume walikuwa ni Wanaafiki!halafu mbaya zaidi
hata Mtume mwenyewe hakuwa akiwafahamu kwa Majina yao!Je sisi
tutawajuaje toba Yaa Rabbi!
Mwenyezi Mungu alimtajia Mtume na
Waislaam kwa ujumla,Sifa za wale Maswahaba wanafiki waliokuwa
wakishirikiana na Makafiri ili kuwagawa Waislaam na wawe makundi makundi
ili Ukafiri uendelee kutawala Duniani.Moja ya Sifa zao ni hii "LAU
WANGELITOKA NANYI WASINGELIKUZIDISHIENI ILA MACHAFUKO,NA WANGELIKWENDA
HUKU NA HUKO KATI YENU ILI KUKUTILIENI FITNA,NA MIONGONI MWENU WAPO
WANAOWASIKILIZA SANA.NA MWENYEZI MUNGU ANAWAJUA MADHALIMU.TANGU ZAMANI
WALITAKA KUKUTILIENI FITNA,NA WAKAKUPINDULIA MAMBO CHINI JUU,MPAKA IKAJA
HAKI NA IKADHIHIRIKA AMRI YA MWENYEZI MUNGU NA HALI WAMECHUKIA"(Sura ya
9 Aya ya 47-48).Naam,ukianzia Aya za nyuma yake utaona namna Wanaafiki
hao walivyokuwa wakihimizwa kwenda kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu nao
wakijitia uzito kwenda,lakini kumbe ilikuwa kheri vilevile kwani hawana
ambalo wangefanya huko Vitani ila kuitia chokochoko na fitna na kuna
hatari ya kuwa wangegawa makundi kwa wengi wao walikuwa wakiwasikiliza
sana wao wanaafiki kuliko Mtume!Na tayari walishampindulia mambo chini
juu!Kwa kuingiza Mafundisho yao ya uwongo na kusema kuwa Mtume ndiye
aliyesema hayo ili kufanikisha mambo yao!kivipi?
"NA WAPO BAADHI YAO
WANAOPINDUA NDIMI ZAO KUKISINGIZIA KITABU ILI MDHANIE KUWA HAYO
YANATOKA KWENYE KITABU,NA WALA HAYATOKI KATIKA KITABU.NA HUSEMA HAYA
YAMETOKA KWA MWENYEZI MUNGU NA HALI HAYATOKI KWA MWENYEZI MUNGU,NA
WANAMSINGIZIA MWENYEZI MUNGU UWONGO NA HALI WANAJUA!"(Sura ya 3 Aya ya
78)
Ndugu zangu,kumbukeni kuwa mambo hayo yalikuwa yanafanywa hali
ya kuwa Mtume mwenyewe yu hai!Sikwambii alipokuja kufa!Yaani Watu
wanatunga mafundisho ya uwongo ili yadhaniwe kuwa nayo ni Mafundisho ya
Mwenyezi Mungu kwa lengo la kuwagawa Waislaam!kivipi?Kwa kutunga
Mafundisho juu ya jambo moja kwa namna tofauti!Utaambiwa kwamba Mtume
Muhammad(s.a.w) alifanya hivi au alitenda hivi!Fundisho ambalo litakuwa
tofauti na fundisho lingine ambalo nalo atakuwa amesema au kutenda
tofauti!ambalo nalo litatofautiana na lingine tena,katika tukio moja!au
kikao kimoja!au mazingira mamoja!na cha ajabu hayo yote yanaweza kuwa
kinyume kabisa na Kitabu kilivyoagiza!
Je ni vipi Mafundisho hayo
yakaja kuwagawa Waislaam baada ya Mtume kufariki na kuwa katika hali
tuionaya hivi sasa!TOA CHOCHOTE UNACHOKIFAHAMU,NA SOMO LITAENDELEA
INSHAALLAH!......
No comments:
Post a Comment