UJUE UISLAAMU HALISI
Sunday, September 2, 2012
SOMO LA MUENDELEZO WA MADHEHEBU
Assalaam
Alaykum, Kumbukeni kuwa
huu ni Uwanja mpana unaruhusiwa kutoa maoni yako kwa namna
ulivyojaaliwa ili mradi usimtukane Mtu wala kumdhalilisha!Ndugu zangu
tutumie Akili na Fikra zetu,laa sivyo tutaenda kuhukumiwa kwa hilo!ALLAH
anasema "NA KWA HAKIKA TUTAWAINGIZA JAHANNAM WENGI KATIKA MAJINI NA
WATU.WANA MIOYO LAKINI HAWAFAHAMII KWAYO,NA WANA MACHO LAKINI HAWAONI
KWAYO,NA WANA MASIKIO
LAKINI HAWASIKII KWAYO.HAO NI KAMA WANYAMA BALI WAO WAMEPOTEA ZAIDI.HAO NDIO WALIOGHAFILIKA"(Sura ya 7 Aya ya 179).
Akasema tena kuwa "HIKI (QUR'AN) NI KITABU TULICHOKITEREMSHA KWAKO ILI
ZIZINGATIWE AYA ZAKE NA ILI WAKUMBUKE WENYE AKILI"(Sura ya 38 Aya ya
29).Na namalizia kwa kauli yake kuwa "......NA(MWENYEZI MUNGU) HUJAALIA
UCHAFU KWA WALE WASIOTUMIA AKILI"(Sura ya 10 Aya ya 100).Aya zote hizo
zinaonesha umuhimu wa utumiaji wa Akili na Fikra zetu katika kuyaendea
mambo ya msingi,kwani ndicho kitu kinachomtofautisha Mwanaadamu na
Wanyama wengine!Haiwezekani wakati wa Usiku Mtu akwambie kuwa huu ni
Mchana nawe ukubaliane nae pasi na kufikiri!
Lakini vilevile,nilitoa
Dondoo za udadisi ambazo zingemsaidia Mchangiaji katika kutoa maoni
yake!Kwamba ikiwa Muongozo umekemea vikali juu ya Madhehebu(Makundi) na
kuiorodhesha kuwa ni Ukafiri na Ushirikina,na ikiwa Mtume(s.a.w)
hakuacha hali ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam!Je nini
kilichosababisha hali hii ya umakundi ndani ya Uislaam?
Dodoso
lingine likasema,Je hali hii ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam
inaweza kuondoka na Dini kurudi kama wakati wa Enzi za Mtume(s.a.w)?
Somo litaendelea inshaallah....!
Akasema tena kuwa "HIKI (QUR'AN) NI KITABU TULICHOKITEREMSHA KWAKO ILI ZIZINGATIWE AYA ZAKE NA ILI WAKUMBUKE WENYE AKILI"(Sura ya 38 Aya ya 29).Na namalizia kwa kauli yake kuwa "......NA(MWENYEZI MUNGU) HUJAALIA UCHAFU KWA WALE WASIOTUMIA AKILI"(Sura ya 10 Aya ya 100).Aya zote hizo zinaonesha umuhimu wa utumiaji wa Akili na Fikra zetu katika kuyaendea mambo ya msingi,kwani ndicho kitu kinachomtofautisha Mwanaadamu na Wanyama wengine!Haiwezekani wakati wa Usiku Mtu akwambie kuwa huu ni Mchana nawe ukubaliane nae pasi na kufikiri!
Lakini vilevile,nilitoa Dondoo za udadisi ambazo zingemsaidia Mchangiaji katika kutoa maoni yake!Kwamba ikiwa Muongozo umekemea vikali juu ya Madhehebu(Makundi) na kuiorodhesha kuwa ni Ukafiri na Ushirikina,na ikiwa Mtume(s.a.w) hakuacha hali ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam!Je nini kilichosababisha hali hii ya umakundi ndani ya Uislaam?
Dodoso lingine likasema,Je hali hii ya Umakundi(Madhehebu) ndani ya Uislaam inaweza kuondoka na Dini kurudi kama wakati wa Enzi za Mtume(s.a.w)?
Somo litaendelea inshaallah....!
MADHEHEBU KATIKA UISLAAM NI USHIRIKINA NA NI UKAFIRI!
Assalaam Alaykum nyote!ndugu zangu hebu leo tuzungumze kuhusu
hili!natanguliza kuomba radhi kwa lugha ngumu ntakayotumia,si kwa nia
mbaya bali ni katika namna ya ufikishaji kwani tukiendelea
kupambapambana kinafiki tutakuwa hatufiki!Sote tunafahamu kuwa Mgonjwa
kama kupona kwake tiba yake ni kuchomwa sindano,japo ataumia ni lazima
achomwe ili kupata uzima wake kama kweli tunampenda!
Madhehebu ni
wingi wa neno Dhehebu ambalo maana yake ni Kundi la jamii ya watu wenye
kufuata mwenendo na mrengo wa namna fulani iliyotofauti na wengine.
Uislaam ni Dini yenye Mfumo maalum ulioelekezwa na Muumba mwenyewe,Mfumo
ambao alimpa Mtume wetu Muhammad(s.a.w) ili naye awafundishe watu.Sote
tunafahamu kuwa Mtume(s.a.w) mpaka anafariki Dunia hakuacha ndani ya
Uislaam Makundi(Madhehebu) katika jamii ya Waislaam.Mtume na wote
waliomfuata walikuwa na mwendo wa namna moja,na wote waliokuwa wakiingia
katika Uislaam aliokuwa akiuhuisha Mtume(s.a.w) walilazimika kushika
mwendo uleule aliokuwa akiufundisha Mtume,NI UPI HUO?
Ni UMOJA wa
kila Jambo katika Dini!Mwenyezi Mungu ni Mmoja(ALLAH),Mtume wetu ni
Mmoja(Muhammad),Kitabu chetu ni kimoja(Qur'an),Dini yetu ni
moja(uislaam).
Mtume(s.a.w) aliwaambia Waislaam "ENYI MLIOAMINI
MUOGOPENI MWENYEZI MUNGU UKWELI WA KUMUOGOPA,WALA MSIFE ISIPOKUWA NI
WAISLAAM.NA SHIKAMANENI PAMOJA KATIKA DINI YA MWENYEZI MUNGU NA WALA
MSIGAWANYIKE!NA KUMBUKENI NEEMA ZA MWENYEZI MUNGU JUU YENU,PINDI
MLIPOKUWA MAADUI BASI AKAZIUNGANISHA NYOYO ZENU NA MKAWA NDUGU KWA NEEMA
YAKE(QUR'AN).NA MLIKUWA KATIKA UKINGO WA SHIMO LA MOTO BASI AKAKUOKOENI
NALO.NAMNA HIVYO MWENYEZI MUNGU ANAKUBAINISHIENI AYA ZAKE ILI MPATE
KUONGOKA!"(Qur'an 3:102-103)
Kwa hiyo Mtume alikuwa akilingania
Umoja baina ya Waislaam wenye utaratibu mmoja,ambapo Mwenyezi Mungu
alimtaka Mtume awakumbushe Historia yao waliokuwa Waislaam kuwa wamekuwa
wamoja,ndugu badala ya hali ya utengano na uadui waliokuwa nao kabla ya
kuwa Waislaam.Kwahiyo Uislaam ulikuwa ni mmoja,kundi moja-Kundi la
Mwenyezi Mungu(Qur'an 58:22) na ni marufuku kuanzisha kundi ndani ya
kundi moja la Uislaam!Bali kulikuwa na kundi lingine ambalo ni kundi la
Shetani ambalo lilikuwa ni dhidi ya Waislaam.
Mara fulani kule
Madina Wanafiki walijaribu kuanzisha Msikiti na wakamuomba Mtume aende
kuuzindua.Mtume(s.a.w) kwa kuwa hakuwa akijua Ghaibu(Siri)
aliwakubalia,lakini Allah mjuzi wa Ghaibu alimkataza Mtume wake asiende
kuuzindua Msikiti huo kwa kuwa waanzilishi wake hawakuwa na lengo zuri
katika kuuanzisha Msikiti huo "NA WALE WALIOTENGENEZA MSIKITI KWA AJILI
YA KULETA MADHARA NA UPINZANI NA KUWAGAWA WAUMINI,NA KUWA SEHEMU YA
KUJIFICHIA YA WALE WALIOMPIGA VITA MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE
ZAMANI......"(Qur'an 9:107).
Ndio kusema kuwa hao walikuwa ni
wanafiki ambao Mwenyezi Mungu aliwaumbua!Kumbe miongoni mwa malengo yao
ni kuwagawa Waumini!wasiwe kitu kimoja kwa manufaa yao binafsi kinyume
na agizo la Mwenyezi Mungu la kuwataka Waislaam wawe ni kitu
kimoja,kundi moja lisilo na mpasuko wala mgawanyiko!Mtume akaambiwa
"USISIMAME KAMWE NDANI YA MSIKITI HUO..."(9:108)
Ndugu zangu njama
za kuwagawa Waislaam zilendelea na kufanyiwa juhudi kubwa tangu enzi za
Uhai wa Bwana Mtume Muhammad(s.a.w).Mtume aliwaasa Waislaam kwa
kuwaambia hali akiwaonya "WALA MSIWE KAMA WALE WALIOGAWANYIKA NA
KUTOFAUTIANA,BAADA YA KUFIKIWA NA UBAINIFU.NA HAO NDIO WATAKAOPATA
ADHABU KUBWA KABISA"(Qur'an 3:105).Kumbe tulishonywa kuwa "Wala tusiwe
kama wale!"Ina maana walikuwepo watu walikuwa wameigawa Dini yao na
wakatofautiana ndani yake!NI KINA NANI HAO?
Hao si wengine bali ni
wale waliopewa Uislaam zamani kisha wakauharibu kwa kuugawa makundi
makundi na kila kundi likawa linajiona liko sawa.Wana wa Israel walipewa
Uislaam kwenye Taurati kupitia Nabii Musa(a.s),wakaugawa Uislaam wao na
ukawa Uyahudi,ambao nao uligawika katika makundi(Madhehebu) ya
Uzayuni,Uothordox,Usquirs n.k.
Baadae wakapewa Injili kupitia Nabii
Isa(a.s),wakauharibu Uislaam wao na waukaufanya kuwa ni Ukristo,ambao
nao uligawika katika makundi(Madhehebu) ya Roman
Catholic,Lutheran,Anglican n.k.
Sasa Waislaam walitakiwa wasiwe kama
hao,wakati huo wao walikuwa ni kundi moja!wakaonywa tena "NYENYEKEENI
KWAKE NA MUMUOGOPE NA SIMAMISHENI SWALA,WALA MSIWE MIONGONI MWA
WASHIRIKINA.AMBAO WAMEIGAWA DINI YAO NA WAKAWA MAKUNDI MAKUNDI,KILA
KUNDI LINAFURAHIA WALIYONAYO"(30:31-32).
Tunapata hitimisho kuwa
kumbe Uyahudi na Ukristo ni Ushirikina kwa kuigawa Dini Makundi
Makundi(Madhehebu).Tena Allah akaonya kwa mara nyingine kuwa "NA
HAWATOKUWA RADHI NAWE MAYAHUDI NA WAKRISTO MPAKA UFUATE MILA YAO.SEMA
HAKIKA MUONGOZO WA MWENYEZI MUNGU NDIO MUONGOZO HASWA,NA KAMA UTAFUATA
MATAMANIO YAO BAADA ELIMU ILIYOKUFIKIA,HUTAPATA KUTOKA KWA MWENYEZI
MUNGU MLINZI WALA MSAIDIZI"(2:120).
Msiba ulioje Waislaam wamefuata
yale waliyokatazwa!Baada ya miaka kadhaa kupita tangu Mtume
kufariki,Waislaam wakagawika Makundi Makundi(Madhehebu)!Mpaka leo hii
Waislaam waliopewa Uislaam katika Qur'an kupitia Mtume Muhammad(s.a.w)
wameugawa Uislaam wao na umekuwa ni Usunni,Ushia,Uanswaar
Sunna,Uahmadiyya n.k. na katika hayo makundi kuna makundi mengine madogo
madogo ndani yake!
Sasa kuhusiana na mambo kama hayo Mtume
aliambiwa na mapema kwamba "HAKIKA WALE WALIYOIGAWA DINI YAO NA WAKAWA
MAKUNDI MAKUNDI HUNA UHUSIANO NAO WOWOTE,BILA SHAKA JAMBO LAO HILO LIPO
KWA MWENYEZI MUNGU,KISHA ATAWAAMBIA YALE WALIYOKUWA WAKIYATENDA"(6:159).
SOMO LITAENDELEA.....
Lakini kwa sasa,Hebu tujadili kwa pamoja,Ni kitu gani
kilichowasababisha Waislaam kuwa na Makundi wakati muongozo wao umekemea
waziwazi tena kwa maonyo makali ya Ushirikina na Ukafiri?.Na
je,Waislaam wanaweza kurudi katika Uislaam mmoja kama alouacha
Mtume(s.a.w)?
UJUE UISLAAMU HALISI
Assalaam
Alaykum,baada ya kuyajua hayo tuliyoyajua kuhusiana na NINI UISLAAM NA
NANI NI MUISLAAM,NA NANI SI MUISLAAM.Leo tuendelee na kipengele kingine
cha maana ya neno DINI.UISLAAM huliangalia neno Dini kwa maana
iliyotofauti na waichukuliayo Wasiokuwa Waislaam!Wasiokuwa Waislaam
hulichukulia neno Dini kwa maana ya Imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi
Mungu.Kwa mfano katika Katika Kamusi ya Kiingereza ya A.S Horbi with A.B
Lowide,A.C Gimson,Oxford Advanced Leaner's Dictionary of current
English,Oxford University Press,Nairobi(1962) Ukurasa wa 713,neno
Religion(Dini) limefasiriwa hivi "Beliefin the existence of Supernatural
ruling power,the Creator and Controller of the universe,Who has given
to Man a Spiritual nature which continues to exist after the death of
the body"
Tafsiri yake ni kuwa "Dini ni Imani ya kuwepo Mungu
Muumba,aliye Muweza na Mwenye Nguvu juu ya kila kitu.Mmiliki wa
Ulimwengu ambaye amempa Binaadamu Roho ambayo huendelea kuishi baada ya
kifo cha mwili"
Aidha katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu neno Dini
limetafsiriwa kama ifuatavyo "Imani inayohusiana na Mambo ya kiroho
baina ya Binaadamu na Mwenyezi Mungu,au njia ya kuhusiana na Mwenyezi
Mungu".Kwa tafsiri hizi Makafiri wao hudai kuwa hawana Dini kwa kuwa
hawana Imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.
Lenin mmoja wa wasomi
wa Kikafiri anasema "Every body must be absolutely free to profess any
Religion he pleases or no Religion whatever,i.e to be a Atheist which
every socialist is as a rule...." Tafsiri yake ni kuwa "Kila Mtu hana
budi kuwa huru kabisa kufuata Dini yoyote anayoitaka au asiwe na Dini
kabisa,yaani awe Kafiri,jambo ambalo inambidi kila mjamaa awe hivyo...."
Neno Dini katika Lugha ya Kiarabu hufasiriwa kama Mila,Utamaduni,Desturi,Njia,Ut ratibu
au Mfumo fulani.Katika Uislaam Neno Dini maana yake ni "Utaratibu au
Mfumo wa Maisha ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu au Kiumbe".Kwa maana hiyo
hakuna Mtu asiyekuwa na Dini kwani ni lazima Mtu awe amefuata utaratibu
fulani ambao aidha amejipangia mwenyewe au amepangiwa!
Na kwa
mtazamo wa Uislaam Dini(Mifumo ya Maisha) ipo mingi tu,ndio maana Mtume
aliambiwa aseme kuwaambia Makafiri kuwa "NYINYI MNA DINI YENU,NA MIMI
NINA DINI YANGU"(Sura ya 106 Aya ya 6).Kwa maana nyingine Mtume alikuwa
akiwaambia kuwa "NYINYI MNA MFUMO WENU WA MAISHA,NA MIMI NINA MFUMO
WANGU WA MAISHA"Tofauti ni kuwa Mfumo aliokuwa akiufuata Mtume umetungwa
na Mwenyezi Mungu mwenyewe na Mfumo waliokuwa wakiufuata Makafiri
walijitungia wenyewe!
"INNAD DIINA INDALLAAHIL ISLAAM..."Mwenyezi
Mungu ananadi kupitia kinywa cha Mtume(s.a.w),yenye Tafsiri kwamba
"HAKIKA DINI INAYOKUBALIKA MBELE YA MWENYEZI MUNGU NI UISLAAM"(Sura ya 3
Aya ya 19).Ukiyakunjua zaidi maneno hayo kwa maana ya neno Uislaam na
neno Dini tulizokwishaziona ni kuwa "HAKIKA MFUMO WA MAISHA UNAOKUBALIKA
MBELE YA MWENYEZI MUNGU NI WAKUTII NA KUNYENYEKEA AMRI,SHERIA NA HUKUMU
ZA MWENYEZI MUNGU"
Na kwa kumalizia somo letu kwa Siku ya
leo,namalizia kwamba "NA ANAYETAFUTA DINI ISIYOKUWA YA
UISLAAM,HAITOKUBALIWA KWAKE.NAYE AKHERA ATAKUWA NI MIONGONI MWA WENYE
HASARA"(Sura ya 3 Aya ya 85).Nayo tukiikunjua inakuwa "NA ANAYETAFUTA
MFUMO WA MAISHA USIOKUWA WA KUTII NA KUNYENYEKEA AMRI,SHERIA NA HUKUMU
ZA MWENYEZI MUNGU,HAUTOKUBALIWA KWAKE.NAYE AKHERA ATAKUWA NI MIONGONI
MWA WENYE HASARA"
Shime ndugu zangu tuishi katika Utaratibu na Mfumo aliouridhia Allah!
"SOMO LITAENDELEA INSHAALLAH......."
Subscribe to:
Posts (Atom)